Why Muranga is Trending

Why Muranga is trending

Screenshot_20230729-180843.jpg


Below is the Full story

BIASHARA ya kununua mbegu za wanaume imenoga katika Kaunti ya Murang’a ambapo baadhi ya wanawake wanalipa hadi Sh300,000 kupachikwa mimba.

Wanaume wanaopendelewa zaidi katika biashara hiyo ni walio na umri wa kati ya miaka 20 hadi 40 lakini wawe wako katika kozi ambazo wanawake hao – Miss Independents – wanaziona ni za watu werevu.

Aidha, wanawake wengi wamesema wanapendelea wanaume warefu na walio na rangi ya ngozi ya wastani, yaani si weupe sana na si weusi kupindukia.

Mwanamke mmoja mjini humo ameambia Taifa Leo kwamba siku hizi wanawake walioamua kushikilia uhuru wao wa kimaisha hawataki usumbufu wa ndoa na badala yake “sisi tunatafuta tu mbegu ili tuzae na kuendeleza kizazi”.

“Lakini katika kuzaa, tunafuatilia sana bahati ya kuwa na watoto wenye sura za kupendeza na pia ubongo stadi wa kuwawezesha kung’ara masomoni,” amesema mwanamke huyo.

Katika hali hiyo, mwanamke aliye katika maamuzi hayo na amefikia awamu ya kusaka mimba anatumana kazi ya kutafutiwa ‘kidume cha mbegu‘.

“Mwanamume huyo ni lazima akubali kupimwa magonjwa hatari ambayo ni ya kizazi na pia yale ya zinaa. Akipita mtihani huo, ni lazima ameze dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi wakati wa ngono na akubali kuhamia kwangu ili asiende kurandaranda huko nje na kuniambukiza ugonjwa,” akasema mdokezi wetu ambaye tayari analea pacha wa umri wa miezi mitatu aliowapata kupitia mradi huo wa kumnunua mwanamume wa kumpachika mimba.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 38 kwa sasa, alimlipa kijana wa umri wa miaka 23 ambaye ni mwanafunzi wa taaluma ya udaktari na ambaye anasomea katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Alimlipa Sh300,000.

“Lakini alipopata habari kuwa nimepata pacha alianza kunidai Sh300,000 za ziada lakini nikamweleza hatukuwa tunauziana watoto bali kazi yake ilikuwa ya kuuza uwezo wa kutunga mimba bila kujali kama ningezaa mtoto mmoja au hata watoto 50 kwa mpigo mmoja,” akasema.

Aidha, ni lazima mwanamume huyo akubali kutia saini kwamba kandarasi yake ni ya kutunga mimba lakini sio malezi na atapoteza uhusiano wake na mtoto na pia mama baada ya kandarasi hiyo kutimiza lengo.

Dkt James Muriithi ameambia Taifa Leo “cha kushangaza ni kwamba wanawake wengi hawajaelewa kwamba werevu wa mtoto kwa kiwango kikubwa zaidi hutegemea ubongo wa mama mzazi”.

Aidha, amesema hakuna kipengele chochote cha kitaaluma ndani ya afya ya uzazi kinachomzima mwanamke kuchagua wa kumpachika mimba bora isiwe ni mwanamume wa chini ya umri wa miaka 18 na pia iwe kwamba tendo linatekelezwa kwa maelewano na wala sio mmoja kumlazimisha mwingine.

Hata hivyo, wakili wa Mahakama Kuu Bw Timothy Mwangi ameambia Taifa Leo kwamba hizo kandarasi za ‘kupachikana mimba’ ni dhaifu kisheria.

“Kandarasi hizo huwa ni za kuzima wauzaji hao wa mbegu kufuatilia uzazi wao ili watoto watambue baba. Wanawake hao hudhania kwamba kandarasi hizo huzima wanaume waliovunwa mbegu kufuata mali kwa kusingizia ndoa,” akasema.

Hata hivyo, Bw Mwangi anasema kwamba Katiba ya Kenya hutambua malezi ya mtoto kuwa ni jukumu la baba na mama.

Anasema kwamba ikiwa mwanamume huyo ataenda mahakamani na ithibitike kwamba yeye ndiye baba mtoto, sheria itatupilia mbali kandarasi ile ya mimba na atambulike kuwa ndiye baba mtoto.

“Lakini tena, sheria inatambua mama kuwa mmiliki wa mtoto hadi afikishe umri wa miaka 18 hivyo basi kumpa uhuru wa malezi isipokuwa katika hali ambapo itathibitishwa mtoto hapati haki zake za malezi bora,” akaeleza Bw Mwangi.

Anaongeza kuwa yule mwanamume aliyezimwa na kandarasi ya mimba kudai umiliki wa mtoto anaweza akashinda kesi ya kutwaa malezi mtoto huyo kama baba mzazi katika hali ya mama kubainika amelemewa kumtunza mtoto.

“Huo ndio mwanya hatari wa kumwezesha mwanamume uliyemlipa kukupachika mimba kuingia katika maisha yako katika siku za baadaye na kupata nafasi hata ya kurithi mali yako kama mshirika wa uzazi,” akasema.

Hata hivyo, anasema wosia pia ukiandikwa na kumnyima baba huyo mali, hali hugeuka kuwa tatanishi na kesi ikiandaliwa mahakamani ya kupinga, huwa ni ngumu sana.

Anamalizia kwa kusema kesi inaweza ikamkana mwanamume huyo au imtambue tu kama baba asiye na haki ya kurithi mali au iamuliwe vinginevyo kutegemea ushahidi ambao huwa umewasilishwa kortini.

mmiliki wa mtoto hadi afikishe umri wa miaka 18 hivyo basi kumpa uhuru wa malezi isipokuwa katika hali ambapo itathibitishwa mtoto hapati haki zake za malezi bora,” akaeleza Bw Mwangi.

Anaongeza kuwa yule mwanamume aliyezimwa na kandarasi ya mimba kudai umiliki wa mtoto anaweza akashinda kesi ya kutwaa malezi mtoto huyo kama baba mzazi katika hali ya mama kubainika amelemewa kumtunza mtoto.

“Huo ndio mwanya hatari wa kumwezesha mwanamume uliyemlipa kukupachika mimba kuingia katika maisha yako katika siku za baadaye na kupata nafasi hata ya kurithi mali yako kama mshirika wa uzazi,” akasema.

Hata hivyo, anasema wosia pia ukiandikwa na kumnyima baba huyo mali, hali hugeuka kuwa tatanishi na kesi ikiandaliwa mahakamani ya kupinga, huwa ni ngumu sana.

Anamalizia kwa kusema kesi inaweza ikamkana mwanamume huyo au imtambue tu kama baba asiye na haki ya kurithi mali au iamuliwe vinginevyo kutegemea ushahidi ambao huwa umewasilishwa kortini.
 
Top